JINSI YA KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MPENZI ALIYE MBALI
JINSI YA KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MPENZI ALIYE MBALI Ni wazi kila mmoja anapenda kufurahia maisha akiwa karibu na mpenzi wake ,hakuna mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake halafu akapenda kuwa naye mbali. Wapendanao hupenda kuwa pamoja wakionana na kujadili mambo mbalimbali huku kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ni jinsi gani anavyompenda. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo iwapo utazitumia kwa umakini basi jua mahusiano yako yatahimili umbali na upendo wako na mpenzi wako utazidi kuwa madhubuti. 1.MAWASILIANO YA MARA KWA MARA Mawasiliano ni moja ya nguzo muhimu sana katika mapenzi zinazofanya mapenzi kuweza kustahimili umbali. Wapenzi wanashauriwa kuwa na kawaida ya kuwasiliana mara kwa mara ili penzi liendelee kuwa na ustawi mzuri,kwan unapokuwa na utaratibu wa kuwasiliana na mpenzi wako mara kwa mara unaufanya ubongo wako usimsahau na kumfanya pia kutambua kuwa unampenda hivyo kujiweka mbali na vishawishi au kumpa nguvu ya kukabiliana navyo. 2.USIWE NA MTAZAMO ...