Mimba Na Imani Potofu

 

Mimba Na Imani Potofu

Mwanadada mmoja alipata mimba baada ya kujamiiana na mpenzi wake mara ya kwanza. Alimpenda sana na hakutaka kufanya ngono kabla ya kuoana. Mpenzi wake alimuomba wajaamiiane , kwanza alikataa lakini baadaye alipewa maneno matamu na hata kulia  kwamba kwa kuwa hataki kujamiiana naye hampendi. Hofu ya kumpoteza mpenzi wake kwa wasichana wengine ilimfanya akubali. Wakati huo alikuwa bikira na alitaka kumthibitishia kuwa anampenda kwa kiasi kwamba anaweza kufanya naye lolote kwa ajili yake. Alijaaminiana naye mara moja ila alijikuta akipata mimba.

Kwa kawaida wanaume wengi hutumia imani potofu kuwashawishi wasichana kujamiiana nao. Hizi ni baadhi ya imani potofu

1) UONGO : Kujamiiana mara ya kwanza na mwanamke bikra hakuna uwezekano wa kupata mimba.
UKWELI : Mwanamke anaweza kupatamimba akifanya mapenzi kwa mara ya kwanza hata kama ni bikra pale tu anapokuwa katika siku zake. Yai la mwanamke litakapokutana na mbegu za kiume (shahawa)

2)UONGO : Kama msichana akikataa kujamiiana na mpenzi wake hampendi
UKWELI : Yapo mapenzi bila kujamiiana. Uhusiano unaweza kudumu bila kijamiana, lakini hauwezi kudumu bila upendo. Kama hauko tayari kujamiiana wasichana waseme hapana kwa ngono.

3)UONGO : Kuosha sehemu za siri na sabuni (mfano Protex) za dawa mara baada ya kujaamiiana kunaua shahawa na kunazuia kupata mimba.
UKWELI : Si sahihi kabisa,hatakama sabuni ingeweza kuua shahawa, ni wazi kwamba msichana hawezi kuosha ndani ya mfuko wa uzazi. Hata hivyo shahawa zinachukua dakika chache kuufikia mirija ya uzazi. Kutumia kemikali kwenye uke  kunaweza kuathiri mwili wa mtu.

4)UONGO : Mimi ni mdogo siwezi kupata mimba
UKWELI : Kwa kawaida msichana anapopata hedhi kwa mara ya kwanza ni ishara kwamba mwili wake umepevuka na anaweza kupata mimba. Hata hivyo msichana anaweza kupata yai kabla ya kuanza kupata hedhi.

5)UONGO : Kuruka-ruka baada ya kujamiiana kunaweza kuzuia mtu kupata mimba.
UKWELI : Hii haisaidii kabisa. Shahawa milioni zinatolewa kwa mara moja. Zinasafiri haraka sana  inachukua muda mfupi kabla ya shahawa hazijakutana na yai la mwanamke na kulirutubisha.

6)UONGO : Kama hakuna mwingiliano hakuna hatari
UKWELI :  Iwapo majimaji ya ukeni na uumeni yatagusana hatari ipo. majimaji yanayotoka kabla ya mshindo yanaweza kuwa na kiasi kidogo cha shahawa ambazo zinatosha kusababisha kupata mimba.

7)UONGO : Ni siku zangu salama za mwezi siwezi kupata mimba
UKWELI : Achilia mbali kubadilika kwa siku za mwanamke kutokana na sababu nyingi kama vile mazoezi magumu, kukosa lishe na hali ya hewa pia wakati wa balehe siku salama ni ngumu. Mzunguko wa hedhi ya wasichana wadogo hautabiriki na hauna uhakika.Shahawa zinaweza kuishi kwa siku tatu hadi nne kwenye mwili wa mwanamke

8)UONGO : Kuchomoa uume kabla ya mshindo ni salama.
UKWELI : Baadhi ya watu hawawezi kudhibiti mvuto wa miili yao na hivyo wanajikuta wakikojoa wakiwa ndani ya uke. Pia majimaji yanayotoka kabla ya mshindo yanakuwa na shahawa zinazoweza kusababisha mimba

9)UONGO : Mwanaume akimeza vidonge vya uzazi wa mpango hawezi kumpa mwanake mimba
UKWELI : Hii si sahihi, dawa hizo zinatengenezwa maalum kwa ajili ya wanawake. Njia sahihi ya kutumia wanaume ni kondom.

10)UONGO : Kama mwanamke/msichana mjamzito akinywa chai ya moto, kichwani na sehemu nyingine  ya mwili wa mtoto itaunguzwa au ngozi inaweza kuwa na mabaki.
UKWELI : Furahia chai yako kwa joto ulipendalo. Mfuko wa uzazi unamlinda mtoto kwa kitu kama hicho. Vizuizi vingine kama wanawake wajawazito wasile mayai na kuku vinawazuia wanawake kufaidi chakula kizuri.

11)UONGO : Kujamiiana wakati wa ujauzito ni kuzuri kwa sababu kunasafisha njia na kumfanya mtoto kuwa .
UKWELI : Si kweli hata kidogo, kinachopatikana hapo ni msisimko wa kawaida utokanao na kujamiiana.Usidanganyike ukifanya ngono kwa imani hii.

Comments

Popular posts from this blog

How To Fight Fair In A Relationship And Grow Closer

Kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Badili Mwenendo wa Maisha yako ya Kingono!